Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amefariki dunia katika ajali ya
Helkopta iliyotokea jana jioni katika eneo la Pori la hifadhi la Selou
Ng'ambo ya mto rufiji.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Operesheni na mafunzo maalumu wa Jeshi la
Polisi,Paul Chagonja aliyekuwepo kwenye uwokoaji huko Selou ameeleza
kwamba Helkopta hiyo imekutwa ikiwa imeungua vibaya na hakukuwepo na
dalili zozote za uwepo wa mtu aliyenusurika.
Awali kabla ya ajali hiyo kutokea Helkopta hiyo iliomba kutua
katika moja ya maeneo ya pori la Selou lakini ilipoteza mawasiliano
kabla ya kutua mpaka ilipoonekana hii leo na inaelezwa kuwa kwenye
helkopta hiyo kulikuwepo na mbunge Filikunjombe,Rubani wa Helkopta hiyo
ambaye ni Captain William Silaa pamoja na abiria wengine wawili ambao
mpaka sasa hivi hawajulikani waliko
No comments :
Post a Comment