Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Mjumbe kutoka China
Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa
kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua
Mkurugenzi mkuu wa MERCHANT International Group ya China
inayojenga bandari ya kimataifa ya BAGAMOYO Dakta HU JIANHUA amesema
ujenzi wa bandari hiyo utakamilika baada ya miaka mitano.
Akizungumza na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimaifa
BERNARD MEMBE kuhusu suala la fidia kwa watu wanaoishi katika eneo la
mradi, Dr. Hu amesema bandari hiyo itajengwa kwa ushirikiano na wadau
wengine wa Oman na serikali ya Tanzania.
Kwa upande wake Waziri MEMBE amesema BANDARI ya KIMATAIFA ya BAGAMOYO
itakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi zaidi ya tano za AFRIKA
MASHARIKI na uzinduzi wa ujenzi wa bandari hiyo utafanywa na Rais
Jakaya Kikwete Kesho mjini Bagamoyo
No comments :
Post a Comment