
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akisindikizwa na Polisi baada ya kuhukumiwa
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius atatoka jela wiki
ijayo na kuhamishiwa kwenye kifungo cha nyumbani, mwaka mmoja baada ya
kuhukumiwa kumuuwa rafiki yake wa kike.
Idara ya magereza ya Afrika Kusini ilisema alhamisi kwamba Pistorius
atahamishwa Oktoba 20 na kuwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa miaka
iliyobaki ya kifungo chake cha miaka mitano.
Pistorius alihukumiwa mwaka jana kwa kumpiga risasi na kumuuwa
mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake Pretoria Februari 2013.
Baraza la kutowa msamaha ilieleza jana kwamba Pistorius atabaki chini ya
usimamizi wa magereza hadi oktoba 20 2019
No comments :
Post a Comment