Timu ya Tanzania Taifa Stars imefuzu kusonga mbele baada ya kufungwa
goli 1-0 na Malawi goli lililopatikana katika kipindi cha kwanza katika
dakika ya 43 ya mchezo goli lililofungwa kifundi nje ya 18 na mchezaji
machachali wa Malawi John Banda anayevaa jezi nambari 7.
Katika mchezo huo uliochezewa katika uwanja wa Kamuzu jijini Blantyre
nchini Malawi, Tanzania ilicheza mchezo wa kujihami huku wakifanya
mashambulizi ya kuvizia wakiwa wamemuacha mbele mchezaji Mbwana Samata
karibu muda wote wa mchezo.
Katika kipindi cha kwa golikipa wa Taifa stars ameokoa magoli mengi ya
wazi kama si umahili wake Tanzania tungekua tunazungumuza vingine sasa.
Ukiangalia kiuchezaji Tanzania haikucheza vizuri kwenye mechi labda
waliingia dimbani wakijua kazi yao ni moja tu ya kulinda magoli yao 2
waliyoyapata kwenye mechi yao ya kwanza iliyochezwa siku ya Juamtano
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar siku ya Jumatano na kuibamiza Malawi
kwa goli 2-0.
Waamuzi walionekana dhahili
wakiipendelea Malawi, kwa mfano kuna mpira wa kurushwa aliutoa mchezaji
wa Malawi lakini kwa mshangao wa wengi wakapewa Malawi kurusha, Pia
Malawi walitoa mpira wa kona baada ya mchezaji Thomas Ulimwengu
kumgongesha mpira beki wa Malawi na kutoka kona mbele ya mshika
kibendera lakini mshika kibendera huyo akaamuru iwe goal Kick. Jambo
lingine ni la refa kutoa kadi za njano kwa wachezaji wawili wa Tanzania
kwa nyakati tofauti kipindi cha kwanza huku akishindwa kutoa kadi za
njano kwa wachezaji wa Malawi kwa makosa kama yale yaliyowapatia
wachezaji wa Tanzania kadi za njano.
Wachezaji wawili wa Tanzania Thomas Ulimwengu na Mbwan Samata walipata
kadi za njano kwa kujitakia wenyewe. wachezaji hawa walichezewa rafu
kwa nayakati tofauti kipindi cha pili karibia na mpira kumalizika lakini
cha ajabu ni kwamba walipoletewa machela ya kuwatoa uwanjani baada ya
kuwa chini kwa muda mrefu walikataa kupanda na kunyanyuka kutaka
kuendelea na mchezo kitu kilichopelekea refa kuwazawadia kadi za njano.
Mpira wa wa Timu ya Taifa ulibadilika mwisho kwenye dadkika ya 76
alipoingia Mrisho Ngassa na kuiongezea uhai safu ya ushambuliaji na
kufanya mpira kuchezewa upande wa Malawi kwenye dakika 10 za mwisho.
No comments :
Post a Comment