Mgombea
mwenza wa urais wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema ),
anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi
(UKAWA), Mh. Juma Duni Haji amewataka watanzania hasa wanaopenda
mabadiliko kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha NLD Dk. Emmanuel
Makaidi kwa kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani Oktoba 25.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kemondo
jimbo la Bukoba vijijini mkoani Kagera Mh. Duni amesema kuwa amepokea
taarifa za kifo cha Dk. Makaidi kwa majonzi makubwa kwani licha tu ya
kuwa ni rafiki yake wa karibu pia alimsaidia sana katika harakati za
kutafuta mabadiliko yanayolenga kuiondoa CCM madarakani kwa kushindwa
kuwaletea wananchi maendeleo huku raslimali zilizopo nchini zikiendelea
kuwanufaisha watu wachache na huduma za kijamii zikizidi kudumaa.
Said Issa Mohammed, Makamu mwenyekiti wa Chadema taifa Zanzibar
anasema kifo cha Dk. Emmanuel Makaidi aliyekuwa mwenyekiti Mwenza wa
UKAWA na mgombea ubunge katika jimbo la masasi mkoani Lindi, kimeacha
pengo kubwa katika medani za kisiasa nchini kutokana na msimamo wake wa
kutetea wanyonge, huku katibu wa jumuiya ya wanawake wa chama cha
wananchi – CUF taifa, Fatuma Kalembo akiwataka akinamama kujitokeza kwa
wingi kwenda kupiga kura siku ya tarehe 25 mwezi huu ili kubadili
mwelekeo wa siasa za Tanzania.
No comments :
Post a Comment