WANANCHI
wa kata ya Urughu,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba hawana huduma ya
Mahakama kwa zaidi ya miaka kumi sasa hali inayochangia kutembea umbali
wa kilomita 27 kufuata huduma hiyo makao makuu ya tarafa hiyo.
Hayo yamebainishwa na diwani wa kata ya Urughu(CCM),Simoni Tyosela
wakati akielezea changamoto wanazopata wananchi wa kata ya Urughu
kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kwao.
Aidha Tyosela ambaye alimaliza muda wake wa uongozi mwanzoni mwa
mwezi huu,alifafanua kwamba tangu alipoingia madarakani mwaka 2010
kipaumbele cha kata hiyo kilikuwa kuhakikisha Mahakama inafanyakazi ili
kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata huduma hiyo umbali mrefu.
Kwa mujibu wa Tyosela walishindwa kuendelea na ujenzi wa Mahakama
baada ya kuagizwa kujenga kituo cha afya na Maabara kutokana na
kaulimbiu ya serikali kwa sasa kuweka kipaumbele ujenzi wa
maabara.licha ya kwamba bajeti ya mwaka wa fedha wa 2015.2016 kwa
kushirikiana na Shirika la HAPA ambao tayari wameonyesha nia ya
kuwasaidia baada ya kuwasilisha maaombi yao.
Akizungumzia malalamiko ya wananchi wa kata hiyo ya Urughu,Hakimu
Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya wilaya ya Iramba,Consolata Singano
alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa Mahakimu wa Mahakama hali
inayochangia wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
No comments :
Post a Comment