Mgombea ubunge wa jimbo la KIJITOUPELE kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi -CCM SHAMSI VUAI NAHODHA
Mgombea ubunge wa jimbo la KIJITOUPELE kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi -CCM SHAMSI VUAI NAHODHA amesema endapo wananchi
watamchagua kuwa mbunge wao atahakikisha anafanya mabadiliko makubwa ya
kimaendeleo.
NAHODHA amesema hayo wakati wa mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Kinuni na kuahidi kuboresha miundombinu.Amesema ataimarisha madaraja ndani ya jimbo hilo ili kuondoa usumbufu wa mafuriko ndani ya Jimbo hilo.
Kwa upande wake mgombea wa uwakilishi kwa tiketi ya CCM jimbo la
PANGAWE, KHAMIS JUMA MWALIMU amesema atajikita zaidi kuimarisha
huduma za jamii.
Hata hivyo amesema jambo lingine ambalo amelipanga kulifanya kama
kiongozi mteule wa jimbo hilo ataanzisha vikundi na kuvisajili kwaajili
ya wanawake ili waweze kupata mikopo.
No comments :
Post a Comment