Mkuu wa mkoa wa MTWARA, HALIMA DENDEGO amewataka wazazi
mkoani humo kuweka mkazo katika suala la elimu na kuhakikisha
wanawapeleka watoto wao shule na kufuatilia maendeleo yao wawapo
shuleni.
DENDEGO amesema mkoa wa MTWARA unafunguka na fursa
za uwekezaji zinazoendelea kujitokeza zinahitaji wataalam katika nyanja
mbalimbali na endapo suala la elimu halitasimamiwa ipasavyo jamii ya
watu wa mikoa ya Kusini itabaki kuwa watazamaji.
Baadhi ya wakazi wa MTWARA wamewashauri wazazi kusimamia kikamilifu
maendeleo ya watoto wao ili washiriki katika ujenzi wa Taifa na kuinua
maisha ya familia kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment