Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - ABDULRAHMAN KINANA
amesema endapo Dkt. JOHN MAGUFULI atachaguliwa kuwa Rais atapunguza
ukubwa wa serikali kwa kuunda baraza dogo la mawaziri.
Akizungumza katika mikutano ya kampeni ya kumnadi mgombea urais kwa
tiketi ya CCM, Dkt. JOHN MAGUFULI mkoani MBEYA, KINANA amesema lengo la
serikali ya awamu ya tano ni kuelekeza fedha kwenye uboreshaji wa
huduma za afya, kilimo na kulipa madeni ya waalimu.Amesema pamoja na kupunguza ukubwa wa serikali pia ataunda baraza
dogo la mawaziri wawajibikaji na wazalendo ambao wataweza kusimamia
ufanisi serikalini.Amewataka wakazi wa wilaya za MBOZI na TUNDUMA kumchagua Dkt.
MAGUFULI ili aharakishe ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji na
kuboresha huduma za afya
No comments :
Post a Comment