Wanajeshi wa Kenya
na Somalia wamefanikiwa kumuokoa mwanamke aliyekuwa ametekwa nyara
katika eneo la Dadaab, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Taarifa ya
msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF) Kanali David Obonyo imesema
Judy Mutua ameokolewa kwenye operesheni ya kijeshi eneo la Shaba-Difu,
kilomita 15 ndani ya Somalia.
Operesheni hiyo imeshirikisha majeshi ya Kenya, kikosi cha polisi wa utawala Kenya, na wanajeshi wa Somalia.
Bi
Mutua, aliyetekwa nyara Oktoba 12 na watu wasiojulikana, anapokea
matibabu na atasafirishwa hadi Nairobi baadaye leo, Kanali Obonyo
amesema.
Ameongeza kuwa mtekaji nyara mmoja ameuawa na mwingine kukamatwa.
Mkuu
wa usalama wa serikali ya Kenya eneo la Kaskazini Mashariki Mohammud
Swaleh amesema Bi Mutua alipelekwa mji wa Dobley kwenye mpaka wa Kenya
na Somalia baada ya kuokolewa.
Ingawa kundi ya al-Shabab halijadai kuhusika katika
utekaji nyara huo, Kanali Obonyo amedai ndio waliohusika katika utekaji
nyara huo kwenye taarifa yake.
Bi Mutua alikuwa akifanya kazi na
shirika shirika lisilo la kiserikali la Windle-trust, moja ya mashirika
yanayohudumu katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, inayotoa hifadhi kwa
takriban wakimbizi 450,000 kutoka Somalia
No comments :
Post a Comment