Ikiwa
imebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida
watu wanne wasiofahamika itikadi zao za kisiasa wame kamatwa na wafuasi
wa chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) kwa madai ya kupita
katika kata za manispaa ya Morogoro na kudai shahada za wapiga kura kwa
nguvu na kuanza kuorodhesha majina ya wananchi na namba zao za simu.
Wakizungumza na ITV baada ya kuwafikisha watu hao katika kituo cha
polisi viongozi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya
Morogoro Jemsi Mkude wamesema watu hao walikuwa wakiwalaghai wananchi
kwa kuandikisha vyama vyao vya siasa, namba zao za shahada za kupigia
kura, namba zao za simu pamoja na kero zinazowakabili kwenye eneo hilo
ambapo wamelitaka jeshi la polisi kutenda haki ilikuepusha uvunjifu wa
amani.
Kwa upande wananchi mashuhududa walio kumbana na watu hao katika
harakati za kuwaandikisha wapiga kura majina wameeleza jinsi watu hao
walivyokuwa wakifanya zoezi hilo kwa kudai kwa lazimima shahada za
kupigia kura ambapo baadhi ya watu walikubali na wengine waifa kwa afisa
mtendaji wakata na wananchi waliamua kuungana na kuwatia hatiani na
kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi cha mji wa Morogoro.
Akitolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo msimamizi wa uchaguzi
jimbo la Morogoro mjini Bi Theresia Mahongo amesema kuwa kufanya hivyo
ni kosa la jinai na kwamba adhabu yake ni faini kati ya shilingi laki
moja hadi laki mbili au kifungo cha miaka miwili ama vyote na kuwaonya
wananchi kuacha kufanya hivyo nikosa la jinai.
No comments :
Post a Comment