Watu 30 wamefariki
baada ya kutokea kwa milipuko miwili katika msikiti ulio karibu na mji
wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa afisa wa
huduma za dharura.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua akiwa
ndani ya msikiti katika mtaa wa Mulai, msimamizi wa Idara ya Kitaifa ya
Usimamizi wa Huduma za Dharura wa eneo hilo ameambia BBC Hausa.
Mshambuliaji wa mbili wa kujitoa mhanga alijilipua watu walipokuwa wakijaribu kutoroka.
Mji huo hushambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika kwenye shambulio hilo lililotokea wakati wa sala ya jioni Alhamisi.
Jumanne, mabomu mengine matatu yalilipuka Maiduguri, na kuua watu wane.
Zaidi ya watu 100 waliuawa katika mashambulio matatu katika mji huo mwezi jana.
Shirika
la habari la AFP Agence France-Presse limesema idadi ya waliofariki
kutokana na shambulio hilo la Alhamisi huenda ikafikia 42
No comments :
Post a Comment