Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema faini ya pauni 50,000 aliyotozwa na chama cha soka cha England (FA) ni fedheha.
Mourinho
amepewa adhabu hiyo ya faini pamoja na marufuku ya mechi moja, ambayo
haitatekelezwa kwa sasa, baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa
nidhamu kufuatia kauli yake kuhusu refa Robert Madley mara baada ya
Chelsea kufungwa 3-1 na Southampton.
Mourinho ameeleza kuwa kutozwa faini hiyo na kufungiwa mechi moja ni kitu cha kushangaza.
Mourinho
pia alimchimba Meneja wa Arsenal Arsene Wenger bila kumtaja jina
alipogusia kuwa Wenger, "alisema nini mara baada ya kuchapwa 2-0 na
Chelsea Mwezi uliopita?".
Wenger alidai refa wa mchezo ule Mike Dean, alikuwa ‘dhaifu’ na ‘asiyefahamu’ soka.
Mbali
na hilo, Wenger pia hakuadhibiwa na FA Oktoba 2014 wakati alipomsukuma
Mourinho, aliyekuwa eneo lake la ufundi, Chelsea ilipopambana na Arsenal
No comments :
Post a Comment