Klabu ya soka ya
Sunderland ya England mwishoni mwa wiki hii wataandika historia katika
sekta ya michezo barani Afrika na hasa katika nchi ya Tanzania.
Klabu
hiyo itafungua kituo cha hifadhi ya michezo kwa vijana wadogo kituo
hicho kilipo eneo la kidongo chekundu Jijini Dar es saalam.
Kituo hicho kitatoa huduma za kimichezo, kielimu na afya kwa wanamichezo chipukizi wanaochipukia nchini Tanzania.
Timu
ya Sunderland imeshirikana na kampuni ya kuzalisha umeme ya Marekani ya
(Symbion Power) kutengeza sehemu hiyo ya michezo itayokua ikiitwa JMK
Youth Park.
kirefu cha jina la kituo hicho ni JMK, ni jina la Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi
wa Sunderland Margaret Byrne, ameiambia BBC wanatarajia kituo hicho cha
michezo kitawasaidia wanamichezo wachanga wa kizazi cha sasa kuendeleza
vipaji vyao.
Kituo hicho kina viwanja vitatu vya nyasi bandia,
kiwanja kimoja cha mchanga, viwanja viwili vya mchezo wa mpira wa
kikapu, huku kukiwa na taa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya michezo ya
usiku.
Uzinduzi wa hifadhi hiyo ya michezo ni mpango ulipo kati
klabu hii ambayo pia inafahamika kama Black Cats na bara la Afrika
katika kufundisha makocha, wachezaji wadogo na kuzijengea uwezo timu za
barani Afrika
No comments :
Post a Comment