Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Dany Ings atakua nje ya uwanja kwa msimu mzima baada ya kuumia goti.
Ings
mwenye miaka 23 aliumia goti wakati wa mazoezi ya klabu ikiwa ni siku
moja tangu atoke kuitumikia timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza,
kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za ulaya dhidi ya timu ya
Lithuania.
Mshambuliaji huyu amefunga mabao matatu katika michezo saba aliyoichezea Liverpool akitokea Burnley.
Ings
anakua mchezaji wa pili kuumia goti baada ya kinda Joe Gomez kuumia
goti na kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima ili kutibu jeraha
lake.
No comments :
Post a Comment