Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kilabu hiyo haiogopi kutumia fedha katika soko la uhamisho.
Raia
huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 60 aliwahutubia washikadau siku
ya alhamisi katika mkutano wa kila mwaka na kukiri kwamba klabu hiyo
ilikuwa na mauzo ya pauni milioni 344 na faida ya pauni milioni 24.7,na
kwamba haina tatizo kifedha.
Arsenal ilimsajili kipa Petr Cech pekee kutoka kilabu ya Chelsea msimu huu.
''Hatuogopi kununua,ninajua nina sifa hiyo'',alisema Wenger.''Iwapo mchezaji ni mzuri tutatumia fedha''.alisema Wenger.
Wenger
alikosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kutomsajili mshambuliaji yeyote
kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho,licha ya kujua kwamba Danny
Wellbeck atauguza jereha hadi krisimasi.
No comments :
Post a Comment