Waathiriwa wa
ugonjwa wa Ebola wametakiwa kutumia mipira ya kondomu hadi kutakapokuwa
na ufahamu wa kutosha kuhusu matokeo ya utafiti yanayoonyesha kwamba
virusi hivyo husalia katika majimaji ya mbegu za kiume kwa kipindi cha
hadi miezi tisa.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa
maambukizi ya ebola kupitia tendo la ngono ni kidogo mno na kutaja
maeneo ya taifa la Sierra Leone ambayo yana idadi kubwa ya manusura
lakini hayana visa vipya vinavyojirudia.
Lakini mkuu wa WHO
Margeret Chan ameiambia BBC kwamba kuna maswali mengi.''Hatujui iwapo
wanaweza kuambukiza ama vipi ,bado hatuna ushahidi wa kutosha''.
''Kiwango
cha ufahamu bado kinatutia wasiwasi ,ndio maana lazima tuchukue
tahadhari ,kwa hivyo tunawashauri manusura kujilinda kupitia mipira''.
No comments :
Post a Comment