Huku Tanzania
ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi wake mkuu wa Oktoba 25, huu hapa ni
wasifu wa Jaji mstaafu Damian Z. Lubuva ambaye amepewa jukumu la
kufanikisha kuendesha na kuhakikisha kuwa uchaguzi huu wa mwaka wa 2015
unaendeshwa kwa njia yenye maadili ya hali ya juu.
Rais Jakaya Kikwete alimteua kwenye wadhfa huo kuchukua pahala palipoachwa wazi na jaji mwenza Lewis Makame aliyestaafu
Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Damian Lubuva Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi alizaliwa Septemba 21 mwaka 1940 katika kijiji cha
Haubi wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Elimu
Alipata Elimu ya Msingi katika shule ya Kuta baadaye katika shule ya Sekondari ya St. Francis (Pugu).
Alijiunga na chuo kikuu cha Afrika Mashariki (Dar es Salaam) alikohitimu na shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1966.
Kazi
Alianza
kazi yake mwaka wa 1966 katika afisi ya mwanasheria mkuu wakati huo
akihudumu kama mwanasheria wa serikali kwa mujibu wa tovuti ya tume
hiyo.
Alijiunga na tume ya kudumu ya Uchunguzi mwaka 1968.
Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, kazi aliyoifanya hadi mwaka 1983.
Aidha aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa nchini Tanzania mwaka wa 1993 kazi aliyoifanya hadi alipostaafu mwaka 2008.
Aliteuliwa kuiongoza tume hii ya taifa ya uchaguzi mwaka wa 2011.
Aliwahi pia kuhudumu kama mwenyekiti wa kamati ya tume ya uchaguzi katika nchi za SADC .
No comments :
Post a Comment