Mgombea
urais wa Zanzibar kwa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharrif Hamad
amesema azma ya seriklai ya CUF endapo itaingia madarakani ni kuigeuza
Zanzibar kuwa ni nchi yenye uchumi mkubwa katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Malim Seif ametoa chmgamoto hiyo huko mkwajuni mkoa wa kaskazini
Unguja katika harakati za mkutano wake wa kampeni za urais
zinazoendelea hapa Zanzibar ambapo amesema tayari amefanya mazungumzo
na wawekezaji wakubwa wa kimatifa nawako tayri kushirikaina na CUF huku
akisema CUF itazindua mpango mpya wa uchumi.
Naye naibu katibu mkuu wa Cuf Zanzibar ambaye ndiye mwenyekiti wa
kampeni za CUF za urais Nassor Ahmed Mazuri amewahakikishia wazanzibari
kuwa serikali ya CUF ikipata ridhaa itafuata sera za rais wa kwanza wa
Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume za kutoa elimu na huduma za afya
bure.
Katika mkutano huo wa Mkwajuni Maalim alipata fursa ya kuwapokea
wanachama waliotoka CCM na kutoa kadi mpya kwa wanchama hao wapatao 39
huku kampeni hizo zikielekea ukingoni ambapo wakati tuneleta taarifa
hizo karatasi za kura kwa uchaguzi huo kwa Zanzibar zinawasili usiku huu
kwa ndege maalum kutoka Afrika Kuisni
No comments :
Post a Comment