Huku joto la
kisiasa likizidi kupanda hapa Tanzania kuhusiana na uchaguzi mkuu wa
urais, agizo la viongozi wa upinzani la kuwataka mashabiki wao wasalie
humohumo vituoni kwa lengo la kulinga kura zao zisiibiwe zimekuwa
zikivutia hisia kali kutoka kwa tume ya uchaguzi.
Tume ilitoa tamko la kuwataka wananchi warejee makwao wakasubiri matokeo ya kura.
Lakini
vyama vikasisistiza kuwa kutokuwepo kwa imani na viongozi wa tume kuu
ya uchaguzi NEC ndiko kuliwalazimu kuchukua mkondo huo ambao NEC imedai
kuwa inakiuka kanuni za upigaji kura.
Rais anayeondoka madarakani Jakaya Kikwete ameingilia swala hilo.
Rais
Kikwete amewaonya vijana dhidi ya kusalia katika vituo vya kupigia kura
kwa dhana kuwa ''wanalinda kura'' akisema wala hilo sio jukumu lao.
''iweje mgombea anasema kuwa eti msalie humo humo vituoni ilikulinda kura ?''
''Tanzania inawapiga kura zaidi ya milioni 22 hawa wote watashinda humohumo vituoni ? Aliuliza Kikwete.
''Hebu tuelewani, hili ni jambo linachekesha sana na halifai kutamkwa na mtu anayewania kuwa kiongozi'' alisema rais.
Awali
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, Jaji mstaafu Damian
Lubuva, alitoa muongozo kamili wa siku ya kupiga kura na akawataka watu
warudi makwao wakasubiri matokeo ya uchaguzi.
Kikwete alikubaliana naye akisema kuwa jukumu la
kulinda kura zisiibiwe litatekelezwa na mawakala wa vyama
watakaoruhusiwa kuingia mle ndani katika vituo vya kupigia kura kwa
ajili ya kupiga msasa kila mpiga kura anayeingia humo kutekeleza wajibu
wake wa kikatiba.
''Mawakala watakuwemo humo kwenye vituo vya
kupigia kura kazi yao nini ?,kazi yao ni kuangilia fulani ameandikishwa
kupiga kura wapi ? anakitambulisho cha taifa ,haya basi anaruhusiwa
kupiga kura katika kituo hicho '' alihoji rais Kikwete
Baadhi ya
vyama vimeshikilia kukutu kuwa kamwe havita fuata maagizo hayo kwasababu
inakiuka katiba ya taifa inayoruhusu watu kusalia takriban mita mia
mbili hivi kutoka kwenye vituo vya kupiga kura.Rais Kikwete alionya kuwa endapo mtu yeyote atajaribu kukiuka sheria hizo basi atakabiliwa na walinda usalama.
Kikwete alikuwa akizungumza baada ya kupokea mwenge wa uhuru huko Dodoma.
Mkurugenzi
wa uchaguzi katika tume ya uchaguzi ya NEC Kailima R. Kombwey alitoa
taarifa ya kuwashauri wananchi wasiingilie maswala ya ulinzi wa kura
kwani maafisa wa kulinda amani watakuwepo.
Viongozi wa upinzani
wamekuwa wakidai kuwa NEC haiaminiki na kwamba itakuwa vigumu vyama
hivyo kuwashawishi wafuasi wao kurudi nyumbani baada ya kupiga kura
ilihali kuna hofu kuwa huenda kura zao zikaibiwa kwa ajili ya kuifaidi
chama tawala.
No comments :
Post a Comment