Takriban maafisa 63 wa kikosi cha polisi nchini Kenya wamefutwa kazi kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.
Msemaji wa polisi ni miongoni mwa wale waliofutwa kazi.Tume ya huduma za maafisa wa polisi iliwafuta kazi maafisa hao baada ya kuwakagua maafisa 1,300 kwa kipindi cha miezi 14.Mbali
na msemaji wa kikosi cha polisi wa utawala Masoud Mwinyi,wengi wa wale
waliosimamishwa kazi wanatoka katika idara ya trafiki.
Mwenyekiti
wa tume hiyo Johnston Kavuludi amesema kuwa wakati wa ukaguzi huo
waligundua kwamba maafisa wa vyeo vya chini wanaofanya kazi katika idara
hiyo walikuwa wakituma kiwango cha fedha wanachopata kwa maafisa
wanaowasimamia kupitia simu zao.
No comments :
Post a Comment