Karatasi za kura za uchaguzi Zanzibar zinatarajiwa kuwasili kesho kutwa
kutoka Afrika Kusini, tume ya uchaguzi Zanzibar-ZEC- imepanga kutumia
shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya uchaguzi mkuu kwa Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa tume ya uchagzui ya Zanzibar
Jecha Salim Jecha wakati akiongea na viongzoi wa vyama vya siasa
ambavyo vinashiriki katika uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar ambapo
amesema maandalizi yanaenda vizuri na hadi sasa wamepatiwa bilioni 2.5
huku akitoa idadi yawapiga kura walioandikisha kwa ajili ya uchagzui na
wapigakura 7743 wamefutwa.Akizungumzia utoaji wa matokeo ya urais mwenyekiti wa ZEC Jecha
Slaim Jecha amesisitiza kuwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo
watatangaza matokeo ya uwakilishi na udiwani ya urais itabakia kuwa ni
jukumu la tume ingawa matokeo hayo yataruhusiwa kubandikiwa ukutani.
Nao badhi ya wagombea urais wa Zanzibar walitoa maoni yao kuhusu
utaratibu wa tume kwenye kura za urais na uangalizi wa wapiga kura Seif
Ali Iddi wa chama cha NRA alihoji tume kutangaza wao huku Kassim Bakari
Alii wa Jahazi asilia alitaka utaratibu wa wangaalizi wa vyama
uangaliwe.
Harakati za uchaguzi Zanzibar zimekuwa zikiendelea kwa kasi ambapo pamoja na kuwepo wagombea 14 wa urais ni CCM na CUF ndio
wanaonekana kuchuana huku kwenye uwakilishi kuna wagombea 181 na
udiwani 346.
No comments :
Post a Comment