Mahujaji
wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali
ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe
24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji
waliofariki dunia.
Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa
Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20).
Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda
Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida
Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat
Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).
Wengine ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab
Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh
Ali (Ahlu Daawa).
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za
mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa
umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2015
No comments :
Post a Comment