Collabo kati ya Diamond Platnumz na producer na rapper mkongwe wa Marekani, Swizz Beatz inakuja
Staa huyo amethibitisha kuwa alizungumza na Beatz kuhusu kufanya wimbo
wao walipokutana New York kwenye tamasha la One Africa Music
“Tulikuwa tunazungumza kuhusu project ambayo tunatakiwa tuifanye,
tuifanye Tanzania au tuifanye wapi, tulikuwa tunaangalia kwa benefit
zote pia,” Diamond aliiambia 255 ya kipindi cha XXL kupitia Clouds FM
“Mimi nilichosuggest nilimuambia ni vizuri tukifanya lakini tuwe na
producer wa Afrika kumix vitu vya Kiafrika na tunaweza tukaifanyia huku
tukatoka nayo tukaenda kuifanyia Tanzania pia sababu itaongeza impact
kwa Afrika na kuonesha wamarekani kweli wanania ya kusaidia muziki wa
Afrika,” aliongeza.
Tayari Diamond amesharekodi collabo nyingine na msanii wa Marekani, Ne-Yo
No comments :
Post a Comment