Maalim Seif ametoa ahadi hiyo huko fumba wakati akiwahutibia wakazi
wa majimbo manane ya wilaya ya magahribi ya kijitoupele, dimani, welezo
na mwankwerekwe na wafuasi wa CUF ambao waliofika kumsikiliza mgombea
huyo ambaye aliwahidi wakazi wa ukanda huo wa magahribi kuwaondoshea
tatizo la maji ambalo wanalo kwa muda mrefu.
Aidha Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais na katibu
mkuu wa CUF taifa alisema katika harakati za kundeleza mjimpya wa fumba
baadhi ya wananchi walipoteza ardhi na haki zao na kutolipwa fidia kwa
mujibu wa sheria hivyo amewahidi kupitia upya madai ya wananchi hao na
kuwalipa madai yao yote.
Katika mkutano huo wa kampeni za urais aliyekuwa waziri na kuwa
kiongozi mwandamizi katika serikali za CCM zilizopita Mohamed Hashim
Ismail amewataka wananchi kuwa makini na kura yao na kutoyumbishwa na
madai ya CCM kuwa imeleta maendeleo.
Kampeni hizo za urais zinaingia katika wiki ya mwisho huku CCM na
CUF zikiendelea na kampeni kila siku ambapo katika wiki hii ya mwisho
kampeni hizo zimekuwa zikiwa unguja pekee.
No comments :
Post a Comment