Akihutubia mikutano tofauti katika vijiji vya Makiungu, Dung’unyi,
Ikungi na Singida mjini, Anna Mghwira ambaye anatumia kauli mbiu ya utu,
uadilifu na uzalendo amesema upepo mkali uliopo katika mkoa huo kwa
mujibu wa tafiti zilizofanywa unaweza kuzalisha umeme na hivyo kupunguza
tatizo la umeme nchini.
Katika hatua nyingine akiwa mjini Singida amemtaka rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na tume ya taifa ya uchaguzi
kuitisha kikao cha wenyeviti wa vyama ili kujadili changamoto hasa
wakati wa upigaji kura na kwamba suala la kukaa mita mia mbili baada ya
kupiga kura ni la kisheria na sio matakwa ya mtu.
No comments :
Post a Comment