Jumuia
za kimataifa, waangalizi wa uchaguzi, wazanzibar na watanzania kwa
ujumla wametakiwa kupuuza ghiliba na propaganda za kuibwa kura
zinazoenezwa na viongozi wa vyama vya upinzani kupitia ukawa kwa kuwa
madai hayo yana ajenda ya siri ya kuvuruga uchaguzi na amani ya nchi
inayopangwa na viongozi hao kwa maslahi yao.
Katika siku ya pili ya kampeni za uchaguzi zinazofanywa kwa pamoja
na Dr Ali Mohamed Shein mgombea urais wa Zanzibar na Dr John Pombe
Magufuli mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika visiwa
vya Zanzibar makamu wa rais wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal anaitoa
kauli hiyo katika viwanja vya mnazi mmoja.
Akizungumza na umati wa wananchi wa Zanzibar waliohudhuria mkutano
huo katika viwanja vya mnazi mmoja Dr John Pombe Magufuli kwa upande
wake mbali na kusisitiza suala la kulinda amani na muungano wa Zanzibar
na Tanganyika serikali yake itaendelea kuzitatua kero nne za muungano
zilizosalia sambamba na kulinda maliasili na rasilimali za taifa
zinazovunwa bila ya kufuata utaratibu.
kwa upande wake mgombea urais wa Zanzibar Dr Ali MohamedSshein
amewataka watanzania kutoyumbishwa katika kudumisha suala la usalama na
amani kwa kuwa ndio ngao pekee ya maendeleo ya taifa.
No comments :
Post a Comment