Baada ya kuona hali hiyo, Dk Magufuli alisema: “Nawaombeni jamani, hatuchagui malaika, kila mtu ana tatizo lake. Inawezekana wengine mmechoka hata kumwangalia, lakini mkitaka mimi nifanye kazi vizuri nileteeni huyu bwana,” alisema akimnadi mgombea huyo.
Kwa nyakati tofauti tangu aanze kampeni mikoani, mgombea huyo amekuwa akiwaambia wananchi kuwa baada ya kumchagua yeye, wawachague wabunge hao na kuwasamehe makosa yao ili apate urahisi wa kuunda Serikali na kuleta maendeleo.
Akiwa Sumbawanga Mjini juzi, Dk Magufuli alimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Aeshi Hilaly kwa kumuita jembe huku akiwataka wananchi “wampigie tena kura hata kama amewakosea.”“Nimesema hatuchagui malaika kila mtu ana kasoro zake. Tuache kasoro, tuangalie maendeleo. Nataka Sumbawanga muwe maalumu mkinichagulia huyu (Aeshi),” alisema Dk Magufuli wakati akihutubia katika Uwanja wa Nelson Mandela juzi.
Katika Jimbo la Kwela – Rukwa, aliwataka wananchi wamsamehe mgombea ubunge, Ignas Malocha kwa makosa aliyowatendea na kuwa atafanya kazi vizuri kwenye utawala wake.
“Tumsamehe, tumjaribu afanye kazi mimi nikiwa rais tuone kama hatafanya kazi
vizuri.”
Hata hivyo, aliposimama katika Kijiji cha Ndalambo wilayani Momba jana, lilizuka kundi la wananchi na kuanza kunyoosha vidole kwa alama ya V inayotumiwa na Chadema na wakati Dk Magufuli akiendelea kumwaga sera wananchi hao waliendelea kupiga kelele na kupinga baadhi ya ahadi kuwa hataweza kuzitekeleza huku wengine wakisema “Lowassa, Lowassa.”

No comments :
Post a Comment