Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemsifu sana mkewe Hillary na kusema anafaa kuongoza taifa hilo.
Kwenye hotuba
yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki mkubwa” na akasimulia
walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma.
Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa
Bi
Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa ujumbe wa
video ambapo alisema: “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa
zaidi katika dari hili la kioo”, akirejelea hotuba ya mkewe Rais Barack
Obama, Michelle, siku ya kwanza ya kongamano.
“Na iwapo kuna
wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa
kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke Marekani na mmoja wenu
anaweza kunifuata.”
Awali, Bi Clinton alisimulia walivyokutana katika Chuo cha Uanasheria Yale mwaka 1971.
“Nilimuoa rafiki yangu mkubwa,” amesema. “Tumekuwa tukitembea na kuzungumza na kucheka pamoja tangu wakati huo.”
Bi Clinton alipitisha wajumbe 2,382 wanaohitajika kutawazwa mgombea baada ya jimbo la South Dakota kutangaza matokeo yake.
Katika
juhudi za kuashiria umoja katika chama, mpinzani wake wakati wa mchujo,
Seneta wa Vermont Bernie Sanders alichukua maikrofoni na kumtangaza Bi
Clinton kuwa mgombea mteule kwa kauli moja, tangazo lililokaribishwa kwa
shangwe.
Awali, wakati wa hotuba yake rasmi Jumatatu, Bw Sanders alikuwa ametangaza: "Hillary Clinton lazima awe rais ajaye wa Marekani.”
Tangazo la Bw Sanders ni kama marudio ya kongamano la 2008 ambapo Bi Clinton alimtangaza Bw Obama kuwa mgombea mteule.
Bi Clinton atakabiliana na mgombea wa Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu Novemba.
Kura za maoni zinaonesha wawili hao wanakaribiana sana kwa uuungwaji mkono wa wapiga kura
No comments :
Post a Comment