Msanii mkongwe wa dansi kutoka kinsasha Koffi Olomide anaendelea kusota jela baada ya juhudi za wanasheria wake kumwombea dhamana kushindikana.
Staa huyo wa muziki wa Lingala alijikuta matatani baada ya kumpiga
teke dancer wake wakati wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi Ijumaa iliyopita.
Polisi wa Kenya walimkamata usiku huo na kumrudisha kwao Kinshasa
hali iliyopelekea kuvunjika kwa show aliyokuwa amepanga kufanya
Kesi yake ilisikilizwa leo huko Kinshasa. Anashikiliwa kwenye gereza la Makala.
“Ni aibu. Ni lazima afurahie haki zake. Mahakama zetu zina kasoro kwa
makosa yaliyofanyika nje ya nchi, hasa kwenye kesi hii. Koffi anajua
ukubwa wa matendo yake na aliomba msamaha. Ataendelea kukaa ndani kwa
walau siku 15,” alisema mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Master Lukoo
Ruffin.
No comments :
Post a Comment