Sakata lakisiasa ambalo linaendelea kuwa gumzo nchini Tanzania limechukua sura mpya baada ya kushuhudia mpambano mkali kati ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.Wakati chadema wakianzisha kampeni yao maarufu kwa jina la UKUTA yaani Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania,wakishiniza kuanzishwa kwa maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia tarehe moja septemba.Raisi Magufuli amenukuliwa akipiga marufuku vikali mikutano ya vyama vya siasa kwa wanasiasa nje ya majimbo yao.President amesisitiza wanasiasa wafanye mikutano ndani ya majimbo yao na si vinginevyo.
"Kila mmoja afanye siasa kwenye eneo alilochaguliwa,Kingu mbunge wa ikungi magharibi afanye mikutano palepale kwake alipoahidi shughuli za maendeleo,Mbowe afanye siasa palepale hai alipochaguliwa na kuahidi kuwapa maendeleo,kila mmoja aliyechaguliwa afanye siasa eneo lake.Sitaki kuona mtu anatoka HAI anakwenda KAHAMA kufanya mikutano n.k Mbunge au Diwani wa HAI au Mbeya anamamlaka ya kuingia kwenye vikao vya maendeleo ndani ya majimbo yao,huwezi kuwa Mbunge wa Ubungo vikao vya maendeleo ukafanyie Tarime.
"Mimi (Rais) pekee ndiye natakiwa kuzunguka nchi nzima kila jimbo kufikisha maendeleo niliyowaahidi watanzania wote.
Wanaotaka kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wanasubiri mwezi wa 9?Wafanye mikutano hata leo ili wajue mimi ni nani.Siwezi kugeuza hii nchi ya siasa,nataka nchi ya maendeleo tu.
Siasa zilishakwisha wakati wa KAMPENI,muda huu ni KAZI TU."
Wanaotaka kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wanasubiri mwezi wa 9?Wafanye mikutano hata leo ili wajue mimi ni nani.Siwezi kugeuza hii nchi ya siasa,nataka nchi ya maendeleo tu.
Siasa zilishakwisha wakati wa KAMPENI,muda huu ni KAZI TU."
Hii ni kauli ya raisi Magufuli alipokua akihutubia wananchi wa mjini Singida leo.
No comments :
Post a Comment